Wednesday, April 23, 2014

Beyonce na Jay Z hawatahudhuria harusi ya Kanye na Kim

Mwezi uliopita (March) kulikuwa na tetetsi kuwa Jay Z ametupilia mpali ombi la Kanye West kumtaka kuwa best man kwenye harusi yake, sasa kuna habari zinazosema kuwa Jay Zhana hat ampango wa kutokea kabisa kwenye harusi yao.
Chanzo kinadai kuw Jay angeweza kutokea kama isingekuwa ni public event, na kuwepo kwa camera nyingi za E pamoja na kutokea kwenye reality show (keeping up with the kardashians).

Matumizi mabaya ya dawa ya kifua kwa asanii yasababisha kutokutengenezwa tena kwa dawa hizo


Kampuni ya kutengeneza dawa za kikohozi"Actavis" yasitisha uzalishaji na mauzo ya dawa za  "Promethazine Codeine" na kuziondoa katika sok, kutokana na matumizi mabaya ya dawa hizo kwa wasanii wengi wakubwa wa Marekani.

Msemaji wa kampuni hiyo amesema kutokana na attention kubwa iliyotolewa na vyombo vua habari Actavis imetoa uamuzi wa kusitisha uzalisha na mauzo ya dawa hizo.msemaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa attention hiyo imeipamba matumizi ya dawa hizo ambayo ni kinyume na sheria na hatari ambayo ni tofauti na matumzi halali ya dawa hizo.

Picha: Wasanii waungana kutengeneza wimbo na video ya wimbo wa muungano

Wasanii zaidi ya 50 wa Bongo Flava, Hip Hop, Injili, Dance na Taarab wameungana pamoja na kufanya wimbo wa kuhamasisha Muungano unaotoka April 26, 2014.

Wasanii wa Tanzania kuanzia muziki, kwaya,dance mpaka bongo movie, wameungana kwa pamoja na kutengeneza wimbo wa pamoja kuhusu Muungano ambao kilele kitakakuwa siku ya ya tarehe 26 mwezi huu.
Wimbo huo umejumiaisha wasanii kama Mabeste, Diamond, Ommy Dimpoz, Lina, Khadija Kopa, Manddojo na Domo Kaya, Mwana FA, AT,AY,Mrisho Mpoto,Madee,Asley,Chege, Qeen Darlin, Mwasitina wengine kibaona kutengenezwa na Tuddy Thomas na kusimamiwa upande wa video na Raqie kutoka I-View Media

Tuesday, April 22, 2014

Chidi Benz ashikiliwa na polisi baada ya kumjeruhi vibaya Ex girlfriend, afikishwa mahakamani

Msanii wa Hiphop anaeiwakilisha Ilala, Chidi Benz anadaiwa kushikiliwa na polisi mwishoni mwa wiki baada ya kumpiga na kumjeruhi vibaya mwanadada anaejulikana kama Mwanaisha  ambae anadaiwa kuwa ni mpenzi wake wa zamani.

Kwa mujibu wa Chidi Benz amesema yeye alikuwa akipita nje ya bar iliyo karibu na kwake ilala Flat alipokuwa akirudi nyumbani kwake akiambatana na mpenzi wake wa sasa ndipo aliposkia sauti ikimuita na kumuuliza zaidi ya mara tatu 

Hatimae Moyes afukuzwa Manchestar

 
Hatimae kocha aliewapa maumivu mashabiki wa Manchester United kwa takriban miezi 10, "David Moyes"amefukuzwa kazi, baada ya kumrithi Kocha anaeaminika saaana Sir Alex Furguson.

United jana walikataa kuthibitisha kuhusu ripoti zilizodai kuwa Moyes angefukuzwa mwishoni mwa msimu.
Moyes (50) aliteiliwa na Sir Alex Ferguson kumrithi wakati kocha huyo (72), alipoamua kustaafu mwaka jana baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 26.

Hizi ndio zasemekana kuwa sababu za ugomvi katika ya Petter na Paul wa Psquare

Mengi yamezungumzwa juu ya kinachodaiwa kutengana kwa kundi maarufu Africa kutoka Nigeria "PSquare" huku wengine wakidai kuwa ni kutokuelewana kwa Petter na kaka yao mkubwa ambae ndio manager wao "Jude Okoye" huku wengine wakitupa lawama kwa mke wa Petter "Lola" kuwa ndio chanzo maana hata mama yao alipokuwa hai hakupenda Petter amuoe mwanamke huyo ambae licha ya kuwa amemuoa baada ya mama yake kufariki, Kaka yake "Jude" hakkuhudhuria harusi yao pamoja na kuwa alikuwepo nchini Nigeria
Leo hii kupitia mtandao wa onlinenigeria umethibitisha sababu za ugomvi mkubwa uliotokea kati ya kaka hao ndugu ambao ni mapacha.

Monday, April 21, 2014

Wema awapoteza Lulu,Jokate,Wolper,Nelly kwenye shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2013-2014


STAA wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ameibuka kidedea kwenye shindano la Ijumaa Sexiest Girl kwa kura 370 huku mshindi wa pili Elizabeth Michael'Lulu' akipata kura 340 akifuatiwa na Nelly Kamwelu.

Shindano hilo lilifanyika katika viwanja Dar Live ,Mbagala usiku wa kuamkia leo  na limeandaliwa na Global Publishers huku burudani ikisindizwa kutoka kwa Weusi(Nikki wa Pili,Joh Makini,G Nako) na Mkubwa na Wanae.Thursday, April 17, 2014

Huu ndio wimbo rasmi wa World cup 2014 "We are one" (Ole Ola) jua wasanii waliopata shavu


Wimbo rasmi wa kombe la dunia mwaka huu umeshatoka na safari hii Pit Bull Jenifer Lopez na Claudia Leitte ndio wamekula shavu la kurecord wimbo huo.
Wimbo huo umeimbwa kwa lugha tatu ambazo ni Kingereza, Kireno na ki-spanis.

Audio: Sikiliza alichokifanya Heri Muziki kwa Jogn Legend


 Daaaaah sidhani kama nina haja kubwa ya kuanza kukuelezea wakati una uwezo mkubwa wa kuingia na kumsikiliza mwenyewe kile ambacho ameamua kukifanya msanii mchanga "Heri Muziki" katika kutaka kukuonyesha uwezo wake mkubwa wa kuimba.....niamini mimi hutajuta. heri amepita mule mule alipopita John Legend kwenye wimbo "All Of Me" ila kama amebadilisha kidogo miondoko na kuitupia katika namba ya kukimbia kidogo na sio ya ku chill kama original version..

DESIGNED

THIS BLOG IS DESIGNED BY DESY ERNEST | PHONE NUMBER : +255-714-890-227 | EMAIL : desy@g5click.com